Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 21:09

Cambodia yapata matumaini ya kufufuka uchumi wake baada ya mikataba ya biashara


Walinzi wakiwa wamesimama mbele ya jengo la NagaWorld huku kukiwa na mgomo wa wafanyakazi huko Phnom Penh, Cambodia, Desemba 22, 2021. (Nem Sopheakpanha / VOA.
Walinzi wakiwa wamesimama mbele ya jengo la NagaWorld huku kukiwa na mgomo wa wafanyakazi huko Phnom Penh, Cambodia, Desemba 22, 2021. (Nem Sopheakpanha / VOA.

Cambodia inaweka matumaini ya kufufuka kwa uchumi baada ya janga kwenye mikataba ya biashara huru  kati ya  China na Korea Kusini, na uanachama katika Ushirikiano kamili wa Kiuchumi wa Kikanda.

Cambodia inaweka matumaini ya kufufuka kwa uchumi baada ya janga kwenye mikataba ya biashara huru kati ya China na Korea Kusini, na uanachama katika Ushirikiano Kamili wa Kiuchumi wa Kikanda.

RCEP ni makubaliano ya biashara huru yakijumuisha wanachama 10 wa Umoja wa Mataifa ya asia Kusini-mashariki, pamoja na China, Japan, Korea Kusini, Australia na New Zealand ambayo yataanza kutumika Januari mosi. Nchi wanachama wa mkataba huo wa biashara wa RCEP zitakuwa na pato la taifa la pamoja la dola trilioni 26.2 , au karibu asilimia 30 ya Pato la Taifa duniani.

Wachambuzi wamesema Phnom Penh ilifuata kwa hali ya juu mikataba hii ya biashara huku kukiwa na athari mbaya ya kiuchumi ya janga la COVID-19 na uondoaji wa baadhi ya manufaa ya kibiashara na Umoja wa Ulaya kutokana na rekodi ya haki za binadamu na demokrasia ya Cambodia.

Waziri wa Mipango Chhay Than amesema zaidi ya ajira milioni 6 katika uchumi usio rasmi zimepotea au zitapotea kutokana na COVID-19, na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa unatarajia kiwango cha umaskini cha Cambodia kinaweza kuongezeka mara mbili hadi kufikia asilimia 17.6 ya watu mwaka huu.

XS
SM
MD
LG