Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:32

Mshukiwa wa mauwaji Cambodia ashitakiwa


Mchambuzi wa kisiasa Kem Ley alieuwawa Cambodia.
Mchambuzi wa kisiasa Kem Ley alieuwawa Cambodia.

Mahakama ya manispa mjini Phnom Pehn Jumatano imemshitaki mshukiwa wa mauwaji ya mchambuzi wa maswala ya kijamii Kem Ley.

Msemaji wa mahakama moja nchini Cambodia amesema kuwa mahakama ya manispa mjini Phnom Pehn Jumatano imemshitaki mshukiwa wa mauwaji ya mchambuzi wa maswala ya kijamii Kem Ley, aliekuwa maarufu kwa kukosoa serikali ya waziri mkuu Hun Sen kwa kosa la kupanga mauwaji na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Msemaji huyo kwa jina Ly Sophanna ameongeza kuwa mahakama hiyo imemshitaki mtu wa pili kwa kusaidia mshukiwa na silaha iliotumika kumuuwa Kem Ley alipokuwa amesimama kununua kahawa kwenye kituo cha kujazia gari mafuta Jumapili asubuhi.

Sophanna hata hivyo hakutoa jina la mshukiwa huyo wa pili hata ingawa vyombo vya habari vimemtambulisha kama Oueth Ang mwenye umri wa miaka 43 na anaeishi Angkor Chum katika jimbo la Siem Reap.

XS
SM
MD
LG