Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 23:34

Bush 41 amezikwa Texas pembeni ya kaburi la mkewe


George Bush akishika jeneza la baba yake mzazi George H.W Bush
George Bush akishika jeneza la baba yake mzazi George H.W Bush

Mwili wake ulisafirishwa kwa treni maalumu hadi mji wa College Station huko Texas na alizikwa kwenye eneo la chuo kikuu cha Texas A&M

Wakazi wa jimbo la Texas nchini Marekani walimuaga Rais wa 41 wa Marekani, George Herbert Walker Bush siku ya Alhamis kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa treni maalumu kuelekea sehemu ya mapumziko yake ya mwisho.

Treni ilianza safari kuelekea mji wa College Station mahala alipozikwa kwenye eneo la chuo kikuu cha Texas A&M. Mara baada ya treni kuwasili ilipokelewa na bendi ya jeshi. Pia jeshi la majini la Marekani lilirusha ndege 21 za vita angani na kutoa saluti kwa nahodha wa majini wa vita ya pili ya dunia ikifuatiwa na ufyatuaji mizinga 21.

George H. W. Bush
George H. W. Bush

George H.W. Bush alizikwa pembeni ya kaburi la mke wake Barbara Bush waliyeishi nae kwa miaka 73. Barbara alifariki mwanzoni mwa mwaka huu.

Hii Ilikuwa mara ya kwanza treni kuubeba mwili wa Rais kwa mazishi tangu mwili wa Dwight D. Eisenhower aliyekuwa Rais wa 34 wa Marekani ulipobebwa na treni kutoka Washington DC kwenda kwenye jimbo lake la Kansas nchini Marekani miaka 49 iliyopita.

XS
SM
MD
LG