Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:07

Mazungumzo ya kuleta amani Burundi yashindikana


wawakilishi katika mazungumzo ya Burundi yalofanyika Uganda December mwaka 2015.
wawakilishi katika mazungumzo ya Burundi yalofanyika Uganda December mwaka 2015.

Juhudi zinazoendelea za kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Burundi zimegonga mwamba baada ya serikali ya Burundi kugomea mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika Arusha Tanzania Jumanne, kutokana na kushiriki kwa viongozi wa upinzani na wa makundi ya kiraia.

Seneta Evelyn Butoyi kutoka ujumbe wa serikali wa Burundi, aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa serikali ya Burundi inakataa kukaa kwenye meza moja na wale wanaowatuhumu kupanga njama za mapinduzi.

Wawakilishi 5 wa vyama viloshiriki katika uchaguzi mkuu wa Burundi, navyo pia viligomea duru ya pili ya mazungumzo yakuleta amani yalofanyika mjini Arusha jumanne, vikisema havikufurahishwa na uwamuzi wa mpatanishi Mkapa kuwaalika waburundi wanaotuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadam na kuhusika katika juhudi za mapinduzi dhidi ya Nkuruzinza hapo Mei mwaka 2015.

Vyama hivyo vya FNL, FROLINA, PIEBU ABANYESHAKA, RADEBU na FRODEBU, vina wasiwasi juu ya kujumuishwa kwa Pacifique Nininahazwe wa chama cha FOCODE, na Armel Ningoyere wa chama cha ACT na Jean Minani katika majadiliano hayo.

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, yanatarajiwa kumaliza mzozo ulioibuka baada ya rais Pierre Nkuruzinza kuwania kuwa rais kwa muhula wa tatu.

Kufwatia kuchaguliwa kwake, ghasia ziliibuka na kupelekea watu takriban elfu 270 kutoroka nchi na wengine zaidi ya 450 kuuwawa.

XS
SM
MD
LG