Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:46

Watoto zaidi ya 50 wameuzwa nchini Burundi nchi za kiarabu


Msemaji wa serikali ya Burundi Alain Nyamitwe.
Msemaji wa serikali ya Burundi Alain Nyamitwe.

Biashara ya watu hasa watoto wa kike ambao hupelekwa katika nchi za kiarabu imeanza kuripotiwa nchini Burundi.

Shirika moja linalodai kupiga vita biashara haramu ya watu linasema kuwa watoto zaidi ya 50 tayari waliuzwa na kupelekwa katika nchi kama Saudi Arabia na Oman. Serikali ya Burundi kupitia waziri wake wa haki za binadamu inaomba wazazi kuwa wawe waangalifu juu ya mbinu zinazotumiwa na wasafirishaji wa watoto hao.

Jumatatu jioni Polisi nchini Burundi ilidai kuwaokoa watoto wanne waliokuwa wakitafutiwa passpoti ili wasafirishwe Jumanne , watoto hao wanne wanatajwa kuwa walikuwa na umri kati ya miaka 15 na 17 , lakini inatajwa kwamba walibadalishwa miaka yao na kuongezwa katika vitambulisho vya bandia.

Kwa mujibu wa shirika la kiraia linalopambana na biashara haramu watoto zaidi ya 50 wa Burundi wamekwishauzwa nje ya nchi tangu 2015.

Hata hivyo maoni ni tofauti nchini Burundi juu ya kazi wanazopewa watoto hao huko Uarabuni baadhi wakisema ni ukahaba na wengine wakidai kuwa wanafanya kazi ya kulea watoto.

XS
SM
MD
LG