Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 22:27

Burundi yawaachia waandishi wa kigeni


Waandishi Jean-Philippe Remy wa Ufaransa na Phil Moore wa Uingereza waliokamatwa Burundi.
Waandishi Jean-Philippe Remy wa Ufaransa na Phil Moore wa Uingereza waliokamatwa Burundi.

Burundi hatimaye imewaachia huru waandishi wa habari wawili wa kigeni waliokamatwa Alhamisi jioni na polisi jijini Bujumbura, Burundi. Hata hivyo vibali vyao vya uandishi nchini humo vimefungiwa.

Philipe Remy mwenye asili ya Ufaransa, mwandishi wa habari wa gazeti la Le Monde la Ufaransa pamoja na Phil Moore mpiga picha raia wa Uingereza walikamatwa na polisi katika kata ya Nyakabiga kati kati ya jiji la Bujumbura wakiwa na vitambulisho halali vinavyowapa ruhusa ya kufanya kazi ya uandishi wa habari nchini humo.

Polisi wa Burundi inawatuhumu kushirikiana na makundi ya watu ambao inasema ni wahalifu.

Hii ni mara ya kwanza kwa waandishi wa habari wa kimataifa kukamatwa na Polisi nchini humo tangu mgogoro ulipoanza mwezi wa Aprili, 2014 baada ya rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kugombea muhula wa tatu.

XS
SM
MD
LG