Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:34

Uchaguzi haukua wa haki Burundi.


Wafuatiliaji wa uchaguzi Burundi wakifautilia matokeo ya uchaguzi uliomalizika hivi karibuni.
Wafuatiliaji wa uchaguzi Burundi wakifautilia matokeo ya uchaguzi uliomalizika hivi karibuni.

Wafuatiliaji wa umoja wa mataifa huko Burundi wanasema kuwa kura za urais ziliopigwa wiki iliyopita hazikuhusisha watu wote na wala hazikuwa huru na zenye haki. Kwenye ripoti ya kwanza iliyotolewa jumatatu, wafuatiliaji hao wamesema kuwa uchaguzi huo uliompa rais Pierre Nkurunziza ushindi wa kuongoza kwa muhula wa tatu wenye utata, ulikuwa na mazingira ya kutokuwa na uhuru na kujieleza kwa waandishi wa habari.

Ripoti hiyo inasema kuwa ingawaje siku ya kupiga kura ilikuwa tulivu, mazingira hayakuwa mazuri ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wenye haki. Rais Nkurunziza ambae alishinda kwa asilimia 69 ya kura zilizopigwa amekumbana na mzozo wa iwapo uongozi wake kwa muhula wa tatu ni wa kikatiba.

Wapinzani wanasema kuwa muhula wa wa tatu ni kinyume cha katiba ilioweka muhula miwili na pia mkataba uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi 2006. Mahakama ya katiba nchini humo iliamuru kwamba rais Nkurunzinza anaweza kugombea tena muhula wa tatu kwa sababu kipindi cha muhula wa kwanza alichaguliwa na wabunge mwaka 2005, na wala sio wapiga kura.

XS
SM
MD
LG