Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 05, 2023 Local time: 17:30

17 wafunguliwa mashitaka ya uhaini Burundi


Polisi wakimwingiza mahakamani mjini Bujumbura Jeneral Juvenal Niyungeko wa jeshi la Burundi, May 16, 2015.
Polisi wakimwingiza mahakamani mjini Bujumbura Jeneral Juvenal Niyungeko wa jeshi la Burundi, May 16, 2015.

Maafisa 17 wa usalama Burundi, ikiwa ni pamoja na majenerali watano, wanaoshutumiwa kwa kujaribu kumpindua Rais Pierre Nkurunziza walifikishwa mahakamani Jumamosi na kufunguliwa mashitaka ya kujaribu mapinduzi.

Washitakiwa hao ni pamoja na majenerali watu wa jeshi na majenerali wawili wa jeshi la polisi, alisema Gervais Abayeho, msemaji wa Rais Nkurunziza. Wengine ni maafisa wa ngazi za chini and wanajeshi wanane. Kiongozi wa jaribio hilo la mapinduzi, Meja Jenerali Godefroid Niyombare, bado hajulikani alipo.

Jaribio hilo la mapinduzi lilikuja huku kukiwa na machafuko nchini humo kuhusu uamuzi wa Nkurunziza kuwania awamu ya tatu ya urais. Baada ya wiki kadha za maandamano mitaani kupinga juhudi za rais kubaki madarakani, Niyombare alitangaza mapinduzi Jumatano.

Nkurunziza wakati huo alikuwa Tanzania kuhudhuria kikao cha dharura cha viongozi wa Afrika mashariki kuhusu hali ya Burundi lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walifanikiwa kuzima jaribio hilo baada ya siku mbili tu.

Wanasheria wanaowatetea washitakiwa hao wa jaribio la mapinduzi wanasema wateja wao wamepigwa na kuteswa wakiwa mikononi mwa polisi.

XS
SM
MD
LG