Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 02:43

Burundi yatia saini mkataba wa Mto Nile


Wahamiaji wakiwa ndani ya meli kwenyeMto Nile, February 15, 2011.

Burundi imekuwa nchi ya sita katika bara la Afrika kutia saini mkataba unaotaka mataifa yashirikiane matumizi ya mto Nile. Hatua ya Burundi inaongeza uwezekano wa kuidhinishwa kwa mkataba huo.

Hivi sasa Misri inadhibiti eneo kubwa la maji ya mto Nile chini ya mkataba wa mwaka 1929. Kama nchi za mto Nile zitaidhinisha mkataba mpya, Misri itapoteza uwezo wake wa kupiga marufuku miradi katika mto Nile iliyopendekezwa na nchi nyingine.

Burundi ilitia saini mkataba ujulikanao kama Nile Basin Initiative siku ya Jumatatu. Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia zilitia saini mkataba huo mwaka jana. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pia imeahidi kutia saini mkataba huo.

Maji ya Mto Nile yanatiririka kupitia au karibu na nchi hizo zilizotajwa kabla ya kuingia Sudan na kisha Misri.

Cairo haijakataa rasmi mkataba huo, lakini ina hofu mpango mpya unaweza kuiacha nchi hiyo bila maji ya kutosha kuweza kuwatosheleza watu wake milioni 80. Sudan pia imeonyesha wasi wasi kwamba mkataba mpya utaiacha nchi hiyo bila kuwa na maji ya kutosha.

XS
SM
MD
LG