Upatikanaji viungo

Wakati dunia ikisherekea mwaka mpya 2016 kwa sherehe na mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ibada hali inaendelea kuwa ya wasiwasi nchini Burundi.

Ripoti zinasema Ijumaa watu 18 wamejeruhiwa akiwemo polisi mmoja jijini Bujumbura katika shambulizi la guruneti lililorushwa kwenye mgahawa mmoja wa pombe katika eneo la Buyenzi.

Polisi nchini humo wameanzisha uchunguzi kujuwa waliohusika na mashambulizi hayo.

Visa vya vurugu na ghasia vimekuwa vikitokea mjini Bujumbura Burundi tangu nchi hiyo ilipoingia katika mzozo wa kisiasa mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka jana.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG