Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 00:49

Burundi yajiandaa kuondoa majeshi Somalia


FILE - Majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kutoka Burundi.
FILE - Majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kutoka Burundi.

Hatua hiyo inafuatia mvutano kati ya Umoja wa Ulaya, ambaye ni mfadhili mkuu wa kikosi cha AMISOM na serikali ya Burundi juu ya utaratibu wa kuwalipa askari wa jeshi hilo.

Serikali imesema kuwa Umoja wa Ulaya hautaki tena serikali ya Burundi kuhusishwa na malipo ya mishahara ya wanajeshi hao.

Hili linatokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyochukuliwa mpaka sasa dhidi ya Burundi tangu mwezi Machi mwaka jana.

Amesema mvutano huo umepelekea wanajeshi hao zaidi ya 5000 kumaliza mwaka bila kupokea malipo yao.

Haijulikani ni lini wanajeshi hao zaidi ya 5000 na vifaa vyao wataanza kuondoka kwenye maeneo wanayosimamia nchini Somalia.

Lakini barua ya mshauri wa rais wa Burundi anayehusika na masuala ya kijamii iliyovujishwa kwa waandishi wa habari, imeeleza kuwa waziri wa mambo ya nje wa Burundi aliamriwa kuufahamisha umoja wa afrika kuwa Burundi itayaondoa majeshi yake iwapo askari wake hawatalipwa mishahara.

Hata hivyo barua hiyo ilisema wadau wote wa Umoja wa Afrika wawe wamepata taarifa hizo kabla ya mkutano mkuu wa marais wa umoja wa afrika uliyopangwa kufanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia tarahe 30 Januari.

Katika barua hiyo pia wizara ya ulinzi inatakiwa kukadiria hasara iliyopatikana kutokana na hali hiyo ya mishahara ya wanajeshi kucheleweshwa.

Msemaji wa rais wa Burundi amesema wakati wakiwapeleka askari hao Somalia taratibu za kisheria zilifuatwa na hivyo hivyo katika kuwaondao ni lazima taratibu zifuatwe ili wasije kudai kuwa hawakujuwa mapema.

Lakini duru za kisiasa zinasema hatua hii ina madhara makubwa kwa Somali.

Mwandishi wetu anasema kuwa sio tu hatari kwa usalama nchini Somalia, pia serikali ya Burundi itapoteza fursa adimu na ya kipekee ya kuingiza sarafu za kigeni.

Tangu machi mwaka jana,Umoja wa Ulaya ulisitisha msaada wa moja kwa moja wa kifedha kwa Burundi kutokana na mzozo wa kisiasa, baada ya Nkurunziza kuamua kugombea muhula wa tatu na kushinda katika uchaguzi wa Julai mwaka 2015 .

Umoja huo unashinikiza serikali ikubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na wapinzani wake, amani ya kudumu ipatikane, haki za binadamu ziheshimishwe.

Mzozo huu wa kisiasa unaoikabili Burundi umepelekea warundi laki tatu kutoroka nchini na ma mia wengine kuuwawa.

XS
SM
MD
LG