Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:25

AU kupeleka washauri wa kijeshi na wafatiliaji wa haki za binadam Burundi


Nembo ya AU
Nembo ya AU

Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini alisema Jumamosi kuwa Umoja wa Afrika utapeleka wafatialiaji wa haki za binadam 100 na washauri wa kijeshi 100 nchini Burundi.

Umoja wa Afrika unasema utapeleka washauri wa kijeshi mia 2 na wafuatiliaji wa haki za binadam nchini Burundi, miezi 10 baada ya mzozo mbaya wa kisiasa kuibuka kufwatia rais Pierre Nkuzinza kuwania muhula wa tatu madarakani. Juhudi za kimataifa za kidiplomasia zinaonekana kupiga hatua chache.

Viongozi 5 wa kiafarika walikuwa nchini Burundi wiki ilopita, wakisukuma kumalizwa kwa mzozo. Matokeo yake yamewashangaza wengine.

Pancase Cimpanye n naibu msemaji wa upande wa upinzani - CNARED - ambaye anaishi uhamishoni.

Bw. Cimpanye anasema,wamevunjika moyo kidogo na ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa sababu haukusisitiza umuhimu wa makubaliano ya amani ya Arusha. Hawakusisitiza juu ya haja ya kufanya majadiliano nje ya nchi, baina ya Nkuruzinza na CNARED, ni maana upinzani, na hawakuzungumza kuhusu vikosi vya umoja wa Afrika.

Mashirika ya haki za binadam, yanasema takriban watu mia 4 wameuwawa katika kipindi cha mzozo huo. Na wengine alki 2 wametoroka nchi.

Mwezi December, Umoja wa Afrika ulipendekeza kupeleka wanajeshi elfu 5 nchini Burundi, lakini baadae waliachana na pendkezo hilo, pale serikali ya Burundi ilipokataa pendekezo lao.

Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini alisema jumamosi kuwa Umoja wa Afrika sasa utapeleka wafatialiaji wa haki za binadam mia moja na washauri wa kijeshi 100 nchini Burundi.

Wafatiliaji hao huwenda wakajiona wana kazi ngumu, anasema mtafiti wa shirika la Amnesty international Rachel Nicholson.

Bi Nicholson anasema,hali nchini Burundi ni tete kwa wakati huu na ni vigumi kwa wafatiliaji wa haki za binadam kufanya shughuli zao. Anasema wameona hali ikizorota haraka katika kipindi cha miezi 10 ilopita, na mwenendo sasa ni kukamatwa kwa vijana hususan kutoka mitaa ya upinzani, hali ya uslama imezorota sana.

Bw Zuma pia alirudia wito wa Umoja wa Afrika wa kufanya majadilano yanayojumlisha pande zote. Serikali ya Burundi inasisitiza kuwa iko tayari.

Upinzani nchini Burundi unasema kuwa chaguo la umoja wa Afrika la mpatanishi, pia huwenda likawa linasitisha mambo.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekuwa akijishughulisha na siasa nchini mwake ambako amekuwa akiwania muhula wa tano madarakani. Shughuli hizo huwenda zikaendelea kwa vile mivutano bado iko juu huko Kampala, kufwatia kukamatwa kwa wagombea wa upinzani na tuhuma za wizi wa kura .

XS
SM
MD
LG