Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 15:41

Burkina Faso yaithibitishia Ufaransa kutaka vikosi vyake kuondoka


Rais wa Burkina Faso, Capt. Ibrahim Traore.
Rais wa Burkina Faso, Capt. Ibrahim Traore.

Serikali ya Burkina Faso, Jumatatu imethibitisha imemtaka mkoloni wake wa zamani Ufaransa kuondoa wanajeshi wake katika nchi hiyo inayo kabiliwa na uasi ndani ya mwezi mmoja ujao, na Paris ilitaka ufafanuzi kutoka kwa kiongozi wa mapinduzi Ibrahim Traore. 

Ufaransa imetuma takriban wanajeshi 400 wa kikosi maalum nchini Burkina Faso inayotawaliwa na serikali ya kijeshi, lakini uhusiano ulizidi kudorora na mivutano imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni.

"Tunasitisha makubaliano ambayo yanaruhusu vikosi vya Ufaransa kuwepo Burkina Faso," msemaji wa serikali Jean-Emmanuel Ouedraogo aliiambia Radio, na Televisheni ya Burkina Faso.

Aliongeza kusema kwamba "huu sio mwisho wa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Burkina Faso na Ufaransa, bali ni jambo la kawaida katika misingi ya makubaliano."

AFP, Jumapili ilipata nakala ya barua ya wizara ya mambo ya nje ya Burkina Faso iliyotumwa Paris, na ilionekana kuwa imeandikwa Jumatano iliyopita, ikiomba kukatisha na kufunga makubaliano hayo ya uwepo wa vikosi vya Ufaransa.

Mjini Paris, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, Anne-Claire Legendre aliiambia AFP kwa maandishi Jumatatu kwamba barua hiyo ilipokelewa kutoka Ouagadougou.

Rais Emmanuel Macron, Jumapili alisema anasubiri ufafanuzi kutoka kwa Traore kuhusu wito wa kujiondoa, akidai kulikuwa na mkanganyiko mkubwa.

Msemaje Legendre alisema Ufaransa bado inasubiri rais wa mpito wa Burkina Faso kutoa ufafanuzi wa barua yake.

Vyanzo kadhaa vilisema Paris ilikuwa ikitafuta uthibitisho kutoka kwa Traore kwa sababu serikali ya Burkina faso imegawanyika kuhusu iwapo wanajeshi wa Ufaransa wabaki nchini au la.

XS
SM
MD
LG