Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 18:06

Burkina Faso yaiomba Ufaransa kuondoa wanajeshi wake ndani ya mwezi mmoja


Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kepteni Ibrahim Traore
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kepteni Ibrahim Traore

Burkina Faso imeiomba Ufaransa kuondoa wanajeshi wake nchini humo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, kulingana na barua ya mamlaka kwa Paris ambayo AFP iliipata Jana Jumapili.

Barua hiyo ya wizara ya mambo ya nje iliyoandikwa Jumatano wiki iliyopita, inahitimisha makubaliano ya mwaka wa 2018 ambayo yaliruhusu wanajeshi wa Ufaransa kupelekwa nchini humo, na kuweka muda wa kikomo wa mwezi mmoja ili wawe wameondoka.

Ilipoulizwa kuhusu barua hiyo, ofisi ya rais wa Ufaransa imesema bado inasubiri uthibitisho wa msimamo wa Burkina Faso kutoka kwa viongozi wa ngaji ya juu.

Mapema Jumapili, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliulizwa kuhusu ombi la Ouagadougou la kutaka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini humo, kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la serikali ya Burkina Faso siku ya Jumamosi.

Macron aliomba taarifa hiyo ichunguzwe kwa makini, akisema kulikuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya matamshi yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari na kusema kiongozi wa kijeshi Ibrahim Traore alitakiwa kutangaza msimamo wa nchi yake.

XS
SM
MD
LG