Kusimamishwa kwa “Jeune Afrique” kuna ashiria kuongezeka kwa ufuatiliwaji wa vyombo vya habari vya Ufaransa toka taifa hilo la Afrika magharibi kuingia katika utawala wa kijeshi mwaka jana.
Taarifa inashutumu gezeti hilo kwa kuvuruga vikosi vya usalama na kutengeneza taarifa ili kuleta taharuki ndani ya nchi kufuatia taarifa mbili zilizo chapishwa katika kipindi cha siku nne zilizopita.
Uhusiano baina ya Burkina Faso na mkoloni wake wa zamani Ufaransa, umekuwa ukizorota toka kuendelea kwa hali ya sintofahamu kuhusu kupungua kwa usalama kunako husishwa na makundi ya wenye msimamo mkali na kusababisha serikali mbili kuondolewa madarakani mwaka jana.
Mvutano umesababisha kufukuzwa kwa maafisa wa kidiplomasia ikijumuisha balozi wa Ufaransa.
Forum