Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 26, 2025 Local time: 18:43

Burkina Faso inatoa wito kuundwa kikosi madhubuti kupambana na ugaidi huko Sahel


Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry
Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa licha ya kuwepo kikosi cha G5 Sahel Joint Force hali iliyosababishwa na ugaidi na ghasia za makabila mbali mbali kwenye eneo inatia wasi wasi

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry anatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutafakari juu ya kuunda ushirika wa kupambana na ugaidi kama ule wa Iraq na Afghanistan ili kupambana na ugaidi kwa njia bora zaidi katika kanda ya Sahel barani Afrika.

Kanda hiyo ya Afrika hivi sasa ina kikosi cha pamoja kiitwacho G5 Sahel Joint Force ambacho kinajumuisha wanajeshi kutoka Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger. Wanajeshi hao wana jukumu la kupambana na kitisho kutoka makundi yenye itikadi kali na yenye silaha. Lakini katika miaka miwili tangu kuundwa kwake jeshi hilo linakabiliwa na kucheleweshwa utekelezaji wa mipango yake na vizuizi ikiwa ni pamoja na kulipuliwa makao makuu yake kwa bomu lililotegwa kwenye gari.

António Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
António Guterres, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa unasema hivi sasa ipo asilimia 75 ya operesheni lakini upungufu unaoendelea wa vifaa na mafunzo unarudisha nyuma maendeleo yake kuelekea operesheni yenye uwezo kamili. Sahel pia ina walinda amani 16,000 nchini Mali na wanajeshi 3,000 wa Ufaransa waliopo nchini Chad kusaidia kurejesha uthabiti.

Lakini licha ya kuwepo kwa vikosi vitatu vya jeshi waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Alpha Barry aliliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba hali iliyosababishwa na ugaidi na ghasia za makabila mbali mbali kwenye eneo inatia wasi wasi.

XS
SM
MD
LG