Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 21:25

Ombi la Zitto Kabwe Bungeni Dodoma lapigwa chini


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania

Bunge la Tanzania limetupilia mbali ombi la Mbunge wa Kigoma Zitto Zuberi Kabwe kupeleka hoja yake binafsi akitaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza madai ya utekaji nyara raia yaliyotokea hivi karibuni wakiwemo baadhi ya waliotekwa kutoka katika Bunge.

Ombi hilo lilisitishwa Jumatano usiku baada ya Bunge kupitisha makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (PMO) kwa kipindi cha 2017/2018 ambayo iliwasilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliopita mjini Dodoma.

Vyanzo vya habari Dodoma vimeripoti kuwa katika kuliwekea uzito ombi lake, Zitto (ACT-Wazalendo) alitumia kanuni 30(4) ya muongozo wa Bunge ambayo inaipa uwezo Bunge kuzungumzia iwapo ipitishe ombi hilo au hapana; kitendo ambacho tayari kilikuwa kimekubaliwa na baadhi ya wabunge, hasa kutoka upinzani, ambao walisimama kuunga mkono ombi hilo.

Alisema kuwa kufuatia mazungumzo na wasiwasi mkubwa wa baadhi ya wabunge wakati wakijadili makadirio ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu madai ya utekaji nyara wa raia, kuteswa na kuuawa kwa raia, itakuwa jambo sahihi kwake kuwasilisha suala hilo binafsi kuhusu kuundwa kwa kamati hiyo kwenye Bunge.

Zitto alidai kuwa Kamati Teule ya Bunge itakuwa na nafasi kuchunguza madai hayo na kutoa ushauri mwafaka na mapendekezo kwa serikali jinsi gani matukio haya ya utekeji nyara yanaweza kudhibitiwa.

Kabla ya kutoa uamuzi juu ya suala hili tata, Spika wa Bunge, Job Ndugai alitaka wabunge kutoa ushauri wao “makini” juu ya hatua bora za kuchukuliwa.

Ilikuwa Tundu Lissu (Singida Mashariki Chadema) ambaye alianza kuchangia, kama kinara wa kambi ya upinzani Bungeni, akieleza kuwa ni muhimu kwa Bunge kulipa suala hili la utekaji nyara mtizamo chanya, akitoa hoja kuwa mazingira yanayofungamana na tatizo hili tayari yamefikia hali mbaya sana.

Alidai kuwa “watu kadhaa” walikuwa wameteswa na kuuawa na kulikuwa na kikosi maalum ambacho kina watu wa kutoka idara za serikali, hasa kati yao ni usalama wa taifa, polisi na jeshi ambao kwa pamoja wanatekeleza vitendo hivyo- nchi nzima.

Mbunge mwengine Halima Mdee (Kawe-Chadema), amesema kuwa Bunge halitakiwi kuzuia hatua ya Zitto katika ngazi hii ya awali… kabla hajapewa “nafasi kutafuta ushahidi zaidi kuhusu tatizo hili.”

Ametoa hoja kwamba itakuwa jambo la busara kwanza kuwasilisha mswada huo, ujadiliwe, halafu- na hapo tu- ndipo wabunge wataweza kuamua kati ya kuukataa au kuukubali.

Ilipofikia hatua hiyo ndipo Spika akamkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Mr George Masaju kutoa mtizamo wa kisheria na tafsiri sahihi ya kanuni iliokuwa imeletwa na Zitto, ni jinsi gani spika ashughulikie tatizo hili “chini ya mazingira yanayoendelea bungeni.”

Katika muhtasari wake alipokuwa anajibu suala hilo, Mwanasheria Mkuu alieleza kwa haraka kuwa wabunge ndio ambao wanatakiwa kufanya uamuzi iwapo wapitishe ombi hili, iwapo hiyo hoja isikilizwe au hapana.

Lakini hata hivyo Mwanasheria Mkuu aliendelea tena kueleza, kwa hali ilivyo hakuna kitu ‘chochote’ cha kujadili kwa sababu serikali tayari iliahidi kufanyia kazi madai hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa), George Simbachawene, alisema hakubaliani na Zitto kuwa ni sawa kwa Bunge kumkubalia yeye kuwasilisha hoja yake ili ijadiliwe.

Kwanza kabisa aliwakumbusha wabunge kuwa serikali ilishajibu madai ya kuwepo kile kilichoelezewa kuwa ni ‘kukundi maalum cha utesaji.’

Lililomuhimu amesema ni kuwa kuna watu kadhaa nchini ambao wamepotea katika mazingira tofauti na serikali imekuwa ikipokea ripoti na maombi kuhusu kuendesha uchunguzi kwenye tatizo hili.

Na ilivyokuwa kwamba serikali imeahidi kushughulikia kero hili, amehitimisha kuwa kuundwa kwa kamati iliopendekezwa itaingiliana na uchunguzi ambao unaendelea.

XS
SM
MD
LG