Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 23:44

Bunge la wazalendo Nairobi lajadili Uchaguzi Mkuu Kenya


Mabango ya uchaguzi katika juhudi ya IEBC kuwaelimisha wapiga kura Kenya

Wakati kampeni zikiendelea Kenya kwa matarajio makubwa ya uchaguzi wa Agosti, watu wanaendelea kukutana siku nzima Nairobi kujadiliana masuala ya uchaguzi.

Inawezekana ikawa hawana uwezo wa kutengeneza sheria, lakini bila shaka wanamaoni kuhusu sheria hizo.

Hapa Nairobi, Bunge la Wazalendo—ambalo ndio “Bunge la Wananchi”—linakutana siku nzima kuzungumzia masuala muhimu na jinsi yatakavyoweza kuwa na athari katika uchaguzi wa August.

“Bila ya shaka tunazungumzia suala la kupanda kwa maisha, na pia tunazungumza kuhusu viongozi wetu wa juu, na pia tunazungumzia takriban kila kitu kinachohusiana na uchaguzi,” amesema mwanaharakati wa haki za kijamii, Margaret Anyango Wayona.

Mwenyekiti wa Bunge la Wazalendo, Gabriel Mayeye amesema:” Huwezi kupata maji, hata kama unahitaji maji hayo, huwezi kupata gari ya wagonjwa kukuchukua hospitali, huwezi kupata huduma ya afya ya bure, huwezi kupata chakula.”

Wananchi kutokana na kukerwa na ufisadi ndiyo imepelekea baadhi ya wapiga kura kumpigia debe Raila Odinga.

Mfanyabiashara mdogo Margaret Nganyi amesema: “Tunangojea kupiga kura ya kumuondoa mtu huyu kwa sababu ni mwizi, ametuibia, anatuchukulia sisi ni watu wa kuburuzwa. Hana muda wa kutuangalia na sisi ndio walipa kodi.”

Lakini wengine wanamsaidia Rais Uhuru Kenyatta, wakitoa sababu kuwa ameleta mradi wa miundo mbinu kama ndio kielelezo cha mafanikio yake.

Alfred Owiti Onyango ambaye ni muuzaji bima ameeleza kuwa “ Kenyatta amefanya kazi nzuri, na bado anasafari ndefu kuwafikisha wakenya mwisho wa safari yao.”

Lakini pia wako wale ambao hawaamini kabisa kwamba chama tawala au upinzani vinaweza kuleta mabadiliko chanya.

Stephen Owoko, mhubiri na aliyewahi kuwa mgombea binafsi wa urais amesema “ kwa hivi sasa, ni suala dogo, ni jambo tu la kusema, yupi ni shetani bora?”

Lakini kitu kimoja ambacho wakenya wengi wanakubaliana.

Wayona ameongeza kuwa “Ilivyo siasa ni kila kitu kwa sababu ukiangalia kile kinachoendelea nchini, kinachochangia katika yote yanayotokea Kenya ni siasa.”

Uchaguzi wa Kenya umepangwa kufanyika August 8. Na wajumbe wa Bunge la Wazalendo watakuwa wanafuatilia kwa karibu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG