Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:03

Bunge la Tanzania kuanza tena vikao vyake Jumanne.


Kikao cha bunge la 11 la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kinaanza tena Jumanne mjini Dodoma ambapo macho na masikio ya watanzania yataelekezwa kusikia mambo kadha wa kadha .

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wananchi wa Tanzania wana shauku jinsi gani wabunge wao watakavyofanikiwa kujadili masuala muhimu ambayo yamekuwa yakigonga vichwa vya habari tangu Rais Joseph Magufuli aanze kazi na kauli mbiu yake ya “Hapa Kazi tu”.

Bunge hilo pia lina sura nyingi za vijana , pamoja na wapinzani chini ya mwamvuli wa muungano wao usio rasmi UKAWA.

Mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar, mwelekeo halisi wa kisiasa wa serikali ya awamu ya tano, hatua ya mabadiliko makubwa ya kamati za bunge,operesheni ya bomoa bomoa jijini Daresalaam na suala la mchakato wa katiba mpya ni miongoni mwa mambo yatakayofuatiliwa kwa karibu.

Bunge hilo linakutana chini ya spika mpya Job Ndugai.

XS
SM
MD
LG