Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 13, 2025 Local time: 09:39

Bunge la Namibia lapitisha sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja


Bendera ya Namibia
Bendera ya Namibia

Wabunge wa Namibia Jumatano wameidhinisha sheria inayoharamisha ndoa za jinsia moja na kuwaadhibu wanaounga mkono ndoa hizo, katika kile wakosoaji wamesema ni shambulio la kinyume cha katiba dhidi ya jamii ya LGBTQ.

Mswaada huo unataka kubatilisha uamuzi wa mahakama ya juu ambao uliruhusu uhalali wa baadhi ya ndoa zilizofanyika nje ya nchi.

Sheria hiyo ilipitishwa na bunge bila upinzani wowote.

“Muungano wa familia ni kati ya mwanaume na mwanamke na hilo lazima liheshimiwe,” Mzee Filipe, mbunge wa chama tawala cha SWAPO aliliambia bunge.

Sheria hiyo inafafanua upya “ndoa” kama muungano “kati ya watu wa jinsia tofauti”.

Inasisitiza kuwa ndoa za jinsia moja zilizofanyika nje ya nchi hazitambuliwi nchini Namibia.

Forum

XS
SM
MD
LG