Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 13:06

Bunge la Marekani lina siku 2 kunusuru serikali kufungwa


Seneta Chuck Schumer (L), akiwa na mdemocratic mwenzie Harry Reid, eneo la bunge, Sept. 27, 2016.

Bunge la Marekani bado halijapata suluhisho siku ya Jumanne la kuepuka kufungwa kwa baadhi ya ofisi za serikali kuu ambapo baraza la seneti limeshindwa kusonga mbele kuruhusu muswada wa muda mfupi wa fedha za matumizi.

Wademocrat walizuia muswada ambao ungeongeza mamlaka ya matumizi ya serikali kuu hadi mwezi Disemba. Vinginevyo bunge lichukue hatua kabla mamlaka kuisha muda wake Ijumaa saa sita usiku siku ambayo ndio mwisho wa mwaka wa fedha wa serikali.

Hatua itakayofuata ni kwamba huduma zisizo za lazima kwa serikali kuu zitafungwa huku ikiwa chini ya wiki sita kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu mwezi Novemba. Warepublican na wademocrat wanalaumiana kila mmoja kwa kusababisha hali hiyo ambayo imeonekana ni kusitisha mwanya wa muswada wa matumizi uliopungukiwa kura 15 zilizohitajika ili muswada kusonga mbele kufika baraza la seneti.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG