Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 22:23

Bunge la Marekani lina siku 12 kuidhinisha matumizi ya serikali kuu


Jengo la bunge la Marekani mjini Washington DC.
Jengo la bunge la Marekani mjini Washington DC.

Bunge la Marekani lina chini ya wiki mbili za kuongeza uidhinishaji wa matumizi ya serikali kuu au kukabiliana na kufungwa kwa baadhi ya ofisi za serikali kuu wakati mwaka wa fedha wa serikali unapoisha hapo Septemba 30.

Huku wamarekani wengi wakilenga kwenye mtazamo wa urais, Washington inaangazia tarehe ya mwisho ya matumizi ya fedha za serikali ambayo itaweza kuwa tatizo kubwa kwa vyama vyote vya kisiasa kama huduma zisizo za lazima za serikali kuu zitakwenda kufungwa wiki kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Washington kwa kawaida inakabiliana na mapambano ya fedha ya mwisho wa mwaka wa fedha wakati wa mwaka wa uchaguzi, lakini mwaka 2016 unaonesha kuwa tofauti pale ambapo wabunge kwa pamoja wanaunga mkono malengo kama vile mapambano ya kirusi cha ZIKA yanayoonekana kuzidi kusambaa.

XS
SM
MD
LG