Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:14

Bunge la Marekani limeidhinisha kuundwa tume huru kuhusu tukio la Januari sita


Jengo la bunge la Marekani
Jengo la bunge la Marekani

Baraza la wawakilishi Marekani, Jumatano liliidhinisha kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza uasi uliotokea kwenye jengo la bunge la Marekani Januari sita 2021 wakati wafuasi wa Trump walipojaribu kuwazuia wabunge kumthibitisha Biden mshindi wa urais

Baraza la wawakilishi linalodhibitiwa na wa Democratic liliungana na wa Republican 35 waliopiga kura 252 kwa 175 ili kuunda tume hiyo, saw ana ile iliyochunguza mashambulizi ya kigaidi yam waka 2001 yaliyofanywa na al-Qaida dhidi ya Marekani.

Lakini hatma ya sheria hiyo bado haijulikani katika baraza la seneti lililogawanyika kisiasa, ambapo kiongozi wa wa republican katika seneti, Mitch McConnell, Jumatano alisema alikuwa akiipinga tume hiyo, siku moja baada ya kusema alikuwa wazi kwa wazo hilo. Sheria za bunge la seneti zingelazimisha wa Democratic kupata kura za wa Republican angalau 10 ili kuanzisha tume hiyo.

Wabunge kadhaa wa Republican, wengi wao wakimtii Trump hata baada ya kupoteza hadhi ya kuwepo White House na kuondoka Washington, wanaelezea kupinga kuundwa kwa jopo ambalo bila shaka litaonyesha jukumu lake la Januari sita kwenye mkutano alioufanya nje ya White House, saa moja kabla ya machafuko kuzuka huko bungeni.

Donald Trump, Rais wa zamani Marekani
Donald Trump, Rais wa zamani Marekani

Trump aliwahimiza maelfu ya wafuasi wake kuandamana kwenda Capitol na kupambana vikali dhidi ya wabunge wakati walipokuwa wanathibitisha ushindi wa Biden kufuatia uchaguzi mkuu wa Novemba 2020, katika mfumo wa kura za wabunge ambazo huamua matokeo ya uchaguzi wa urais Marekani.

Kiasi cha waandamanaji 800 waliofanya ghasia, wengi wao wakiwa wamevaa kofia na mashati yenye maandishi ya Trump, waliwashambulia maafisa wa zamani huko Capitol, walivunja madirisha na milango, wakachukua udhibiti wa vyumba vyote huko bungeni, walichakura kwenye makaratasi, katika ofisi za bunge, na wakapambana na polisi, kabla amri kutolewa baadae, ya kurejesha hali ya utulivu. Watu watano walikufa, na zaidi ya 400 wamekamatwa tangu wakati huo na kufunguliwa mashtaka ya makosa ya jinai.

XS
SM
MD
LG