Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:00

Bunge la Marekani lapinga kura ya turufu ya Rais Obama


Jengo la bunge la Marekani
Jengo la bunge la Marekani

Bunge la Marekani limepiga kura ya kupinga kura ya turufu ya Rais Barack Obama ya muswada ambao unaruhusu kufunguliwa mashtaka dhidi ya Saudi Arabia kwa mashambulizi ya ugaidi yaliofanyika Septemba 11 mwaka 2001.

Kura ya Jumatano kutoka pande zote bungeni zilikuwa za idadi ya juu. Ilikuwa mara ya kwanza kwa kura ya turufu ya bwana Obama kupingwa.

Kura zilikuwa 97 kwa 1 katika baraza la seneti, ambapo kiongozi wa walio wachache kwenye chama cha Democratic, Harry Reid wa jimbo la Nevada, ndio mwanachama pekee aliyeungana na Rais. Kura ya wabunge zilikuwa 348 kwa 77.

Matokeo hayo ni ushindi mkubwa kwa familia za watu waliouwawa katika mashambulizi ya ugaidi ya Septemba 11 mwaka 2001. Hadi hivi sasa juhudi zao za kutafuta sharia katika mahakama za Marekani zimekuwa zikikwamishwa kutokana na Saudi Arabia kuwa na kinga ya kisheria.

Rais Obama alikiambia kituo cha televisheni cha CNN nchini Marekani kwamba uamuzi wa bunge kuruhusu hatua ya kuendelea kufunguliwa mashtaka kwa nchi hiyo ni makosa.

XS
SM
MD
LG