Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:38

Bunge la Kenya lajadiliana kutatua mgomo wa madaktari


Mgomo wa madaktari nchini Kenya unaelezewa kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaotegemea huduma za afya katika hospitali za umma
Mgomo wa madaktari nchini Kenya unaelezewa kusababisha vifo kwa wagonjwa wanaotegemea huduma za afya katika hospitali za umma

Tayari kuna ripoti za vifo kutokana na mgomo wa madaktari unaondelea nchini humo

Bunge la Kenya limelazimika kufanya mjadala maalumu kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea nchini humo.

Madaktari na wauguzi waliamua kugoma kufanya kazi kuanzia mapema jumatatu wakidai nyongeza ya mishahara na marupuru ambayo walitakiwa kupewa na Serikali.

Wananchi nchini Kenya wamelaani kitendo hicho cha madaktari na wauguzi kugoma wakidai kuwa kinahatarisha maisha ya watu. Tayari kuna ripoti za watu waliokufa kutokana na mgomo huo.

Lakini madaktari wanasema hakuna njia nyingine ya kushinikiza ili waweze kulipwa fedha zao isipokuwa kuikumbusha serikali kwa kutumia mgomo.

Wakati huo huo Bunge la Kenya limeruhusu majeshi yake kuungana na yale majeshi ya Umoja wa Mataifa ya Uganda na Burundi au AMISON, ili kupambana na vitendo viovu vya kundi la Al shabab la nchini Somalia.

Kundi la wanamgambo wa Al Shabab limefanya mashambulizi na utekaji nyara kadhaa wa wageni katika ardhi ya Kenya.

XS
SM
MD
LG