Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 21:36

Bunge la Kenya lajadili uwezekano wa kujitoa ICC


Bunge la Kenya lajadili uwezekano wa kujitoa ICC

Bunge la Kenya Jumatano limejadili suala la uwezekano wa kujiondoa kwenye mkataba wa mahakama ya kimataifa ya ICC.

Wakili wa masuala ya kisheria na mkuu wa idara ya kupambana na rushwa nchini Kenya PLO Lumumba ambaye amesema kuwa ikiwa Kenya itataka kujiondoa kwenye ICC ni lazima watoe ilani ya mwaka mmoja.

Kwahiyo ameongeza hata kama Kenya itatoa ilani mambo ambayo yameanza bado yataendelea na pia amegusia katika katiba mpya kwamba ibara ya pili kwamba sheriza zote za kimataifa ambazo Kenya imeidhinisha itakuwa ni sehemu ya sheria za Kenya.

Kumekuwa na mjadala kwenye bunge la Kenya unaopamba moto kuhusu uwezekano wa kujitoa kwenye mkataba wa ICC.

Pia kumekuwa na hoja kwa baadhi ya wabunge kudai kuwa kujadiliwa suala hilo kwenye bunge ni kinyume cha katiba.

Plo Lumumba alizungumza na sauti ya Amerika juu ya uwezekano huo wa Kenya kujitoa.

XS
SM
MD
LG