Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 11:48

Bunge la Kenya lachunguza wizara ya kigeni kwa ubadhirifu


Rais Mwai Kibaki akihutubia kikao cha ufunguzi cha bunge la Kenya
Rais Mwai Kibaki akihutubia kikao cha ufunguzi cha bunge la Kenya

Bunge la Kenya linatarajiwa kuendelea na kikao cha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na ulaji rushwa dhidi ya maafisa wa wizara ya mambo ya nchi za nje na waziri wao Moses Wetang'ula siku ya Jumanne.

Mkuu wa kamati ya masuala ya ulinzi na ya kigeni bungeni Bw. Adan Keynan aliwasilisha kwa masa mawili stakbadhi na ushahidi wa kudhihirisha jinis waziri Wetang'ula na maafisa wa vyeo vya juu wa wizara yake walihusika katika ubadhirifu na wizi wa fedha za umaa katika kununua ardhi kwa ajili ya ujenzi wa balozi za Kenya huko Tokyo, Nigeria, Ubelgiji, Misri na Pakistan.

Bw Keynan ametoa hoja ya kumtaka Bw Wetang'ula na katibu mkuu wa wizara Thuita Mwangi kuondolewa au kujiuzulu wakati uchunguzi unaendelea. Waziri anabidi kueleza ilikuaje walinunua ardhi ya kujenga ubalozi wa Kenya Tokyo nje kidogo wa mji huo kwa thamani ya Shs bilioni 1.75 za Kenya wakati ilikua ni yenye thamani ya Shs milioni 450 za Kenya.

Waziri huyo anatazamwa kueleza pia juu ya jinsi sehemu ya fedha kununua ubalozi wa Kenya nchini Misri imepotea. Na kwanini gharama za ujenzi wa ubalozi huko Islamabad zilipanda karibu maradufu na kazi haijakamilika. Kwa upande wa Nigeria fedha zilizouzwa ubalozi wake huko Lagos ilipohamishwa mji mkuu mpya wa Abuja hazijulikani zimepotea wapi.

Uchunguzi huo unafuatia uwamuzi wa Rais Mwai KIbaki na waziri mkuu kumsitisha kazi waziri wa elimu ya juu Bw. William Ruto kwa tuhuma za ulaji rushwa. Spika wa bynge Kenneth Marende ameahirisha kikao hadi jumanne.

XS
SM
MD
LG