Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:41

Bunge la EAC kuwaadhibu wanachama wasiolipa michango


Ramani ya Afrika Mashariki
Ramani ya Afrika Mashariki

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) limelitaka Baraza la Mawaziri kuchukua hatua kali ikiwemo kuziwekea vikwazo nchi wanachama zisizotimiza wajibu wake wa kutoa mchango wa fedha, kulingana na katiba ya jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya jumuiya Burundi inadaiwa dola milioni 13, Tanzania dola milioni 9, Kenya Dola milioni 8, Rwanda dola milioni 7 na Uganda dola milioni 2.

Bunge hilo Jumatano, limetaka Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuelezea changamoto ya uhaba wa fedha unaoikabili sekretarieti hivi sasa na kuzihimiza nchi wanachama kutoa michango yao kwa wakati ili kufanikisha shughuli za jumuiya.

Sudan Kusini, ambayo ni mwanachama wa jumuiya hiyo, imepewa muda wa hadi mwisho wa mwezi wa Oktoba, 2019 kuwasilisha malimbikizo ya michango yake ya dola milioni 27.

Hoja hiyo imeibuka baada ya hivi karibuni Jukwaa la Asasi za Kiraia katika ukanda Afrika Mashariki (EACSOF) kutaka kufungua shauri katika mahakama ya jumuiya hiyo kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu uhalali wa wanachama wasolipa ada zao kuendelea na uanachama wao.

XS
SM
MD
LG