Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:30

Bunge la DRC lapiga kura ya kumtimua waziri wa uchumi.


Barabara za mji mkuu wa DRC Kinshasa zikionekana kuwa tupu wakati wa masharti makali ya kupambana na janga la Covid 19, Aprili 19, 2020. Picha ya Reuters.
Barabara za mji mkuu wa DRC Kinshasa zikionekana kuwa tupu wakati wa masharti makali ya kupambana na janga la Covid 19, Aprili 19, 2020. Picha ya Reuters.

Bunge la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatano limepiga kura ya kumuondoa kwenye wadhifa wake waziri wa uchumi Jean Marie Kalumba, likimshtumu kwa mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu na uratibu mbovu wa sekta ya uvuvi, kati ya masuala mengine.

Waziri huyo amepewa saa 48 ili awe amekwisha wasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia kura hiyo ya kumuondolea imani.

Kalumba aliteuliwa kwenye wadhifa huo na Rais Felix Tshisekedi mwaka jana.

Hoja iliyotiwa saini na wabunge imeweka wazi malalamiko mengi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa sera ya kusaidia wavuvi na uhaba wa petroli wa mara kwa mara unaosababisha ongezeko la bei ya usafiri.

Kalumba hakupatikana mara moja kwa ajili ya maelezo.

Congo ni mzalishaji mkubwa wa shaba barani Afrika na mchimbaji mkubwa wa madini ya betri ya cobalt duniani, lakini inasalia kuwa mojawapo ya nchi maskini zaidi zenye maendeleo duni duniani.

XS
SM
MD
LG