Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:06

Wabunge Croatia wapiga kura kutaka bunge ivunjwe


Waziri Mkuu wa Croatia, Tihomir Oreskovic.
Waziri Mkuu wa Croatia, Tihomir Oreskovic.

Bunge la Croatia limepiga kura leo Jumatatu kuvunjwa na kutoa njia ya uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Septemba.

Wabunge 137 waliunga mkono hoja la kulivunja bunge hilo huku wawili wakipinga na mmoja kutopiga kura.

Upigaji kura umetokea wiki moja baada ya wabunge kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Tihomir Oreskovic kwa kura ya kutokuwa na imani nae.

Kazi ya mwisho ya bunge hilo itakua ni Julai 15.

Croatia, mwanachama mpya wa Umoja wa Ulaya, imekuwa ikikumbwa na mvutano wa kisiasa na kukwama kwa utekelezaji wa mageuzi ya kiuchumi kwa wiki kadhaa sasa.

XS
SM
MD
LG