Sheria hiyo inapiga marufuku vyombo vya habari vya ndani kupokea ufadhili au msaada wa vifaa wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja kutoka nje, chini ya tishio la kufunguliwa mashtaka ya uhalifu ikiwemo faini ya hadi dola 15,000.
Inakubali kuwa siri ya kitaalamu ni haki, lakini inaruhusu mahakama kuwalamizisha waandishi wa habari kufichua vyanzo vyao.
Inapiga pia marufuku kwa watu wenye uraia pacha kumiliki vyombo vyote vya habari au sehemu ya vyombo hivyo, na waandishi wa habari wanaofanyia kazi vyombo vya habari vya kigeni bila kibali, wanaweza kutozwa faini ya dola 7,600.