Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:14

Bunge la 11 nchini Tanzania kuanza rasmi shughuli zake Jumanne


Wabunge katika bunge la zamani la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma.
Wabunge katika bunge la zamani la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodoma.

Bunge la 11 la serikali mpya ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Magufuli linatarajiwa kuanza rasmi Jumanne mjini Dodoma kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Oktoba 25 mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bunge hilo linatarajiwa kuwa na matukio kadhaa ikiwemo upatikanaji wa spika na naibu wake lakini pia linatarajiwa kuthibitisha jina la Waziri Mkuu wa Tanzania kama litakavyowasilishwa na Rais Magufuli.

Mjini Dodoma mchakato wa kumpata spika kwa upande wa chama tawala ambacho ndicho chenye wabunge wengi umekuwa ukiendelea kupitia vikao mbalimbali vya chama hicho ambapo kamati kuu ya CCM ilipitisha majina matatu kati ya wanachama wake 22 walioomba nafasi ya uspika ambayo yalikuwa nia Job Ndugai, Dk. Tulia Akson na Abdulla Mwinyi .

Taarifa zilizopatikana Jumatatu mjini Dodoma hata hivyo zilieleza kuwa katika kikao cha wabunge wote wa CCM kilichokaa kupitia majina ya hayo matatu ya wagombea nafasi ya uspika, wagombea wengine wawili walijitoa na kumwachia Job Ndugai, na hivyo kumfanya kuwa mgombe pekee wa nafasi hiyo kutoka Chama Cha Mapinduzi-CCM.

Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodomaanzania Parliament
Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini Dodomaanzania Parliament

Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa, bwana Nape Nnauye alitoa ufafanuzi juu ya hatua iliyofanyika kwa chama cha CCM hatimaye kumpata mgombea mmoja tu wa nafasi ya kiti cha spika.

Bwana Job Ndugai ambaye alikuwa naibu spika katika bunge lililopita alielezea matumaini yake ya kuongoza bunge la 11 kutokana na ukweli kwamba Chama Cha Mapinduzi-CCM chenye wabunge wengi wanatarajia kushinda uchaguzi huo wa spika dhidi ya vyama vingine vya upinzani vitakavyosimamisha wagombea.

Ratiba ya Jumanne baada ya kuanza kikao cha kwanza cha bunge na kusomwa tangazo la rais la kuitisha bunge, inaonyesha kufanyika kwa uchaguzi wa spika na kisha ataapishwa na baada ya tukio hilo wabunge wataanza kuapishwa, shughuli itakayoendelea hadi alhamis asubuhi na baadaye alhamis jioni wabunge watathibitisha jina la Waziri Mkuu kabla ya Rais mpya Dr.magufuli kulihutubia bunge Ijumaa alasiri.

XS
SM
MD
LG