Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 16:21

Bunge la EA lapitisha sheria ya mazingira


Maporomoko ya katika mto Nile
Maporomoko ya katika mto Nile

Mswada wa Afrika Mashariki wa mazingira yanayovuka mpaka ambao ulianza kujadiliwa mwaka wa elfu mbili na kumi hatimaye umepitishwa.

Mswada huo wa sheria ulopitishwa Kampala siku ya Alhamisi unalenga kuhifadhi mazingira haswa kwenye maeneo ambayo yanavuka mpaka ya nchi wanachama.

Wabunge wanapendekeza kuundwa kwa tume ambayo itakagua kazi zote za Serikali ya nchi fulani ikiwa Serikali hii itaanzisha shughuli zozote zile kwenye maeneo fulani ambayo yanavuka mpaka na ambayo yanaweza kuathiri nchi jirani. Tanzania iliupinga mswada huu kabla ya kupitishwa.

Mswada wa Afrika Mashariki wa mazingira yanayovuka mpaka ambao ulianza kujadiliwa mwaka wa elfu mbili na kumi hatimaye umepitishwa lengo likiwa kuhifadhi mazingira.

Tanzania haikuunga mkono asilimia mia moja mswada huu.

Marais wa nchi za Afrika Mashariki wanatarajiwa kuuridhia mswada huu kabla ya miezi mitatu ijayo kumalizika. Ikiwa watauridhia, basi mswada huu utakuwa sheria mara moja.

Kwa muda wa wiki mbili sasa, bunge la Afrika Mashariki limekuwa likifanya vikao vyake mjini Kampala.

XS
SM
MD
LG