Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:21

Buhari aapishwa rasmi rais mpya wa Nigeria


Rais mpya wa Nigeria, Mohammadu Buhari katika sherehe za kuapishwa kwake mjini Abuja, Mei 29,2015
Rais mpya wa Nigeria, Mohammadu Buhari katika sherehe za kuapishwa kwake mjini Abuja, Mei 29,2015

Rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari anasema Nigeria haiwezi kujitangazia ushindi juu ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram bila ya kuwaokoa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara mwaka jana kutoka mji wa Chibok.

Bwana Buhari alisema katika hotuba yake baada ya kuapishwa Ijumaa kwamba wasichana 219 waliotekwa April mwaka 2014, lazima waokolewe. Aliliita kundi la Boko Haram lisilojali, haliabudu mungu na haliendani na imani ya ki-Islam.

Mohammadu Buhari
Mohammadu Buhari

Bwana Buhari ambaye amemrithi Goodluck Jonathan ni m-Nigeria wa kwanza kushinda kiti cha rais katika uchaguzi mkuu kwa kumtoa rais aliyeko madarakani. Alikula kiapo cha kuingia madarakani wakati wa sherehe katika mji mkuu Abuja zilizogubikwa na mabango yakionyesha bendera ya Nigeria yenye rangi ya kijani na nyeupe.

Katika hotuba yake ya kula kiapo Buhari alisema anataka Nigeria kuchukua jukumu la kusimamia uongozi wa eneo ambapo alisema ni matarajio ya Afrika. Nigeria ni nchi yenye idadi kubwa ya watu katika bara la Afrika na inaongoza uzalishaji wake wa mafuta.

Pia alikiri matatizo ya kiuchumi Nigeria ambayo yanajumuisha ongezeko la watu wasio na ajira na kiwango kikubwa cha umaskini na pia aliahidi kukabiliana na tatizo sugu la upungufu wa umeme katika siku za mbeleni.

Muhammadu Buhari na John Kerry (R)
Muhammadu Buhari na John Kerry (R)

Sherehe hizo zilihudhuriwa na darzeni za wakuu wa nchi. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry aliongoza ujumbe kutoka Marekani.

Rais Goodluck Jonathan aliyemaliza muda wake madarakani pia alihudhuria sherehe hizo, alikuwa akitabasamu na alivaa vazi lake la siku zote linaloendana na kofia akiwa amesimama pembeni na mrithi wake kabla ya kula kiapo.

Goodluck Jonathan(L) na Muhammadu Buhari (R)
Goodluck Jonathan(L) na Muhammadu Buhari (R)

Alhamis bwana Jonathan alimkabidhi bwana Buhari mlolongo wa maelezo juu ya urais na alimuonyesha maeneo kuzunguka makazi ya rais katika kuonyesha kwamba wanakabidhiana madaraka katika mazingira ya amani.

Bwana Buhari anakabiliwa na masuala makubwa kama vile kutapakaa kwa rushwa na ghasia za kundi la Boko Haram katika eneo la kaskazini nchini Nigeria matatizo ambayo Rais Jonathan hakuweza kuyatatua.

XS
SM
MD
LG