Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 18:15

BRICS yasema itafuata mfumo wa biashara wa WTO


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa BRICS Johannesburg, Afrika Kusini,Julai 25, 2018.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa BRICS Johannesburg, Afrika Kusini,Julai 25, 2018.

Viongozi wa mataifa matano yenye uchumi unaokua haraka duniani maarufu kama BRICS, wametoa tamko la pamoja kuunga mkono uwazi na ushirikiano wa mfumo wa biashara ya kimataifa ulioainishwa na Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Viongozi hao kutoka Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini wameweza kufikia kauli moja inayohamasisha biashara ya kimataifa katika mkutano ho wa siku tatu, wakiahidi kupambana na ubinafsi wa kibiashara wakati ambapo kuna vitisho vya ushuru vilivyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.

Viongozi hao wamekiri kuwa biashara ya kimataifa inakabiliwa leo na changamoto nyingi kufuatia hatua za Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua hatua kadha za kuziwekea ushuru bidhaa muhimu kutoka China na mataifa ya Ulaya.

"Tunatambua kuwa mfumo wa biashara za kimataifa unakabiliwa na changamoto ambazo hazijawahi kutokea. Tunasisitiza umuhimu wa kuwa na uchumi wa dunia uliokuwa wazi," tamko hilo lililokuwa limesainiwa na viongozi watano limesema.

XS
SM
MD
LG