Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 02:24

BRICS: Mataifa yakutana kipindi cha mageuzi duniani


Mkutano wa BRICS unaowaleta pamoja viongozi wa mataifa yanayo chipukia kiuchumi –Urusi, India, China na Afrika Kusini umeanza Jumatano mjini Johannesburg Afrika Kusini na utadumu kwa siku tatu

Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Urusi Vladimir Putin, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Brazil Michel Temer wanahudhuria kikao hicho cha kila mwaka pamoja na baadhi ya viongozi wa Afrika walioalikwa.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa katika mazungumzo kati ya Xi na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Jumanne walisema mkutano huo wa Johannesburg una umuhimu mkubwa kwa ushirikiano wa BRICS.

Mapema Julai China na Marekani wote waliwekeana ushuru katika bidhaa zenye thamani ya jumla ya bilioni 34 ikiwa ni mwendelezo wa mvutano wa kiuchumi.

Tangu wakati huo Marekani imetangaza mpango wa kuwekea ushuru bidhaa zaidi za China zenye thamani ya Dola bilioni 200.

Vyanzo vya habari vimesema kuwa China imesema ushuru huo wa Marekani ni "ukandamizaji" na mwanzo wa "vita vikubwa zaidi vya kibiashara katika historia".

Lakini sio kwamba mahusiano ya China ni mazuri sana wakati Xi akiwa tayari amewasili Afrika Kusini kwa mkutano huo.

Mkutano huo umekuja katikati ya mabadiliko yanayotokea ulimwenguni, moja ni lile linaloilenga hasa China juu ya vita vya kibiashara vinavyoendelea, ambapo Rais wa Marekani Donald Trump anatishia kuweka ushuru wa bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 505 ambayo China inaziuza Marekani.

Nayo China ikijibu hatua hiyo ya Marekani imesema itafanya juhudi ya kujenga ushirikiano na mataifa mengine, kama yale yaliyoko katika BRICS, ambapo kuna mazingira mazuri zaidi ya kibiashara, kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya China-Africa Cobus Van Staden.

XS
SM
MD
LG