Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 02:14

BREXIT: Waziri wa Leba ajiuzulu


Aliyekuwa waziri wa leba na malipo ya uzeeni wa Uingereza Amber Rudd
Aliyekuwa waziri wa leba na malipo ya uzeeni wa Uingereza Amber Rudd

Hali ya kisiasa nchini Uingereza iliendelea kuzorota Jumapili, kufuatia kujiuzulu kwa mmoja wa mawaziri wa ngazi ya juu katika serikali ya Boris Johnson.

Waziri wa Wafanyakazi na Malipo ya Uzeeni, Amber Rudd, aliuacha wadhifa wake Jumamosi na kudai kwamba Waziri Mkuu Johnson hafanyi vya kutosha katika kutafuta muafaka unaostahili kabla ya nchi hiyo kujiondoa kwa umoja wa ulaya (Brexit).

Rudd alisema hajaona ushahidi wowote kuwa Johnson anatafuta makubaliano yoyote kabla ya tarehe ya mwisho iliyowekwa ya nchi hiyo kuondoka kabisa kwa umoja huo.

katika barua yake ya kujiuzulu, waziri huyo alisema serikali ya Johnson inatumia muda na raslimali nyingi kujitayarisha kuondoka kwa umoja huo bila makubaliano yoyote, na kwamba hajaona kiwango kama hicho cha shauku, katika kutaka mazungumzo na umoja wa ulaya.

Aliyekuwa waziri wa leba na malipo ya uzeeni wa Uingereza Amber Rudd
Aliyekuwa waziri wa leba na malipo ya uzeeni wa Uingereza Amber Rudd

Haya yamejiri siku mbili tu, baada ya kakaye waziri mkuu, Jo Johnson, kujizulu wadhifa wake wa ubunge, na kutangaza kwamba ameachana na siasa.

Wachambuzi wamitaja hatua hiyo kama pigo kubwa kwa kiongozi ambaye aliahidi wafuasi wake kwamba angefanya maamuzi ya busara kuliko mtangulizi wke, Theresa May, ambaye alizulu wadhifa wa Waziri Mkuu baada ya kushindwa kuwaleta Wingereza pamoja kuhusiana na suala hilo la Brexit.

Aidha, Johnson anakabiliwa na changamoto kubwa ya kisiasa kufuatia baadhi ya wabunge wa chama chake cha Conservative kupiga kura wakiunga mkono wenzao wa Labor, wanaopinga msimao wake kwamba, liwalo na liwe, Uingereza itaondoka kwa Umoja wa Ulaya hata kama makubaliano ya kibiashara kati yake na Brussels hayatakuwa yameafikiwa.

XS
SM
MD
LG