Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:25

Brazil yashuhudia ongezeko la moto kwenye msitu wa Amazon mwaka huu


Moto kwenye sehemu moja ya msitu wa Amazon mapema wiki hii
Moto kwenye sehemu moja ya msitu wa Amazon mapema wiki hii

Takwimu rasmi zilizotolewa Jumatatu na idara ya anga za juu za Brazil INPE, zinaonyesha kwamba idadi ya mioto ya mwituni mwaka huu imepita ile ya mwaka jana.

Hali hiyo inaonekana kuwa tishio kubwa kwenye msitu wa Amazon ambao ni wenye mvua nyingi zaidi ulimwenguni. Picha za satellite kuanzia Januari mosi hadi mwezi huu zimeonyesha jumla ya mioto 75,592 ikiwa idadi kubwa kulinganishwa na 75,090 mwaka uliopita. Ripoti hiyo ya karibuni zaidi huenda ikaathiri rais Jair Bolsonaro ambaye anawania tena uongozi kwenye uchaguzi mwezi ujao, huku pia akikabiliwa na shutuma kali za kimataifa, kutokana na uharibifu wa msitu wa Amazon.

Wataalam wanalaumu Bolsonaro kwa kulegeza kanuni zilizokuwa zikilinda msitu huo kutokana na wakataji haramu wa miti, pamoja na wafugaji tangu alipochukua madaraka 2019. Kufikia sasa hakuna tamko lolote kutoka kwa ofisi ya Bolsonaro wala wizara ya mazingira ya Brazil. Msemaji wa shirika la kimazingira la Greenpeace nchini humo Andre Freitas ametaja takwimu zilizotolewa kuwa janga lisilo na kifani.

XS
SM
MD
LG