Kwa takriban mwaka mmoja wasichana wadogo wameweza kujiunga na kikundi cha maskauti watoto.
Lakini kuanzia Ijumaa, wasichana wenye umri kati ya miaka 11-17, wanaweza kushiriki katika programu za Boy Scouts, ambayo hivi sasa inajulikana kama Scouts BSA.
Mtaala wao wa mafunzo ni njia ya kufikia daraja ya kiwango cha juu katika klabu hiyo inayojulikana kama Eagle Scout.
Vikundi vinavyo jumuisha wasichana na wavulana, hata hivyo haviandaliwi na Scouts BSA. Hivi sasa wavulana na wasichana wataweza kupata vyeo kwa kadiri ya juhudi zao kwa usawa na kuweza wote kufikia vyeo vya juu.
Kwa mujibu wa tamko la Boy Scouts of America katika tovuti yao, “Uongozi wa BSA unaamini kuwa njia bora ya kuwakaribisha wasichana na kuweza kuzitumikia familia za wakati huu ni kutoa viongozi ambao wanatokana na mfumo uliokuwepo wa jinsia moja uliokuwa tayari na faida mbalimbali zilizo thibitishwa, lakini wakati huohuo kutoa nafasi ya uongozi kwa wasichana na wavulana.
Facebook Forum