Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:37

Botswana yamlaumu Kabila kwa ghasia DRC


Rais wa Congo, Joseph Kabila akiwa Kinshasa, Januari 26, 2018
Rais wa Congo, Joseph Kabila akiwa Kinshasa, Januari 26, 2018

Nchi ya Botswana siku ya Jumatatu ilimlaumu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Joseph Kabila kwa matatizo ya kibinadamu na usalama nchini mwake katika ukosoaji mkali kabisa kutoka serikali ya kiafrika kwa kiongozi huyo kukataa kwake kujiuzulu.

Mataifa ya magharibi yamerudia mara kwa mara kumkosoa bwana Kabila ambaye muhula wake wa kuwa madarakani uliisha tangu Disemba mwaka 2016 lakini mataifa ya kiafrika yanachukulia suala hilo taratibu wakipendekeza utaratibu kuelekea uchaguzi uliocheleweshwa kwa muda mrefu lakini wanaepuka kumlaumu moja kwa moja Kabila.

Malori ya jeshi la DRC yakibeba raia wanaokimbia ghasia
Malori ya jeshi la DRC yakibeba raia wanaokimbia ghasia

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilijikombowa mwaka 2003 kutoka vita vya miaka mitano ambavyo mamilioni ya watu walikimbia nchi hiyo na mamilioni kuuliwa, wengi kutokana na njaa pamoja na magonjwa, na mzozo wa kisiasa uliopo hivi sasa umechangia mgogoro mkubwa ambao umewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia nyumba zao.

Angalau watu 22 wakiwemo raia 15 waliuwawa katika siku mbili zilizopita katika mapambano ya kikabila huko mashariki mwa Congo katika jimbo la Kivu kaskazini, ofisa mmoja alisema.

XS
SM
MD
LG