Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 20:54

Mlipua bomu Boston apewa adhabu ya kifo


Kundi la wanajeshi wa zamani wakipinga adhabu ya kifo mbele ya mahakama ya Boston, May 15, 2015.

Mlipua bomu wakati wa mashindano ya mbio ndefu za Boston marathon April 2013, Dzhokar Tsarnaev, amepewa adhabu ya kifo baada ya kupatikana na hatia katika kesi yake wiki kadha zilizopita. Shambulizi hilo la bomu liliuwa watu watatu na kujeruhi wengine 264.

Baraza la wazee wa mahakama mjini Boston lilibaini kuwa kitendo cha shambulizi hilo kilistahili adhabu ya kifo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Fatima Tlisova aliyekuwa ndani ya mahakama hiyo aliandika ujumbe wa twitter akisema "baadhi ya wazee wa baraza la mahakama walikuwa wakitokwa na machozi, Tsarnaev aliinamisha kichwa."

Baraza hilo kwa pamoja lilifikiwa uamuzi huo, ama sivyo adhabu yake ingekuwa kifungo cha maisha bila uwezekano wa msamaha.

Tsarnaev mwenye umri wa miaka 21 alikutwa na hatia ya mashitaka 30 yanayohusiana na ugaidi.

XS
SM
MD
LG