Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 12:34

Boris Johnson 'ameanza kampeni' kuwa waziri mkuu wa Uingereza


Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Gatwick karibi na London Okt 22, 2022
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Gatwick karibi na London Okt 22, 2022

Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amerudi nchini humo katika juhudi zake za kujaribu kurudi madarakani baada ya kujiuzulu wa Liz Truss.

Johnson alilazimika kujizulu baada ya utawala wake kukumbwa na sakata za kimaadhili.

Truss aliondoka madarakani Alhamisi wiki hii, baada ya kuwa waziri mkuu kwa muda mwa wiki sita tu, wanasiasa kadhaa wameanza matayarisho ya kugombea nafasi hiyo.

Johnsona alikuwa katika visiwa vya Caribbean kwa likizo, nafasi ya waziri mkuu ilipotangazwa kuwa wazi, amerejea Uingereza na kuanza kutafuta uungwaji mkono.

Darzeni ya wabunge wa chama cha Conservative wametangaza kumuunga mkono.

Anahitaji kuidhinishwa na wabunge 100.

Waziri wa biashara James Duddridge amesema kwamba Johnson amemwambia kwamba atagombea tena nafasi ya waziri mkuu.

Shirika la habari la Sky News, limeripoti kwamba abiria waliokuwa kwenye ndege moja na Johnson akirudi Uingereza, walimkejeli na kumfanyia mzaha.

Wachambuzi wa siasa za Uingereza wamesema kwamba litakuwa tukio la kipekee iwapo Johnson, ambaye alikuwa mwandishi wa habari na meya wa London, atarejea madarakani.

Wagombea wa nafasi ya waziri mkuu

Aliyekuwa waziri wa ulinzi Penny Mordaunt, alikuwa wa kwanza kutangaza nia ya kuwania wadhifa wa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Boris Johnson na aliyekuwa waziri wake wa fedha, Rishi Sunak wametajwa kuwa wagombea wakuu katika kinyang’anyiro hicho.

Upigaji kura ndani ya chama cha Conservative kumtafuta kiongozi mpya wa chama, ambaye atakuwa waziri mkuu, utafanyika wiki ijayo.

Sunak, alimaliza wa pili nyuma ya Liz Truss katika uchaguzi uliopita. Hajatangaza rasmi iwapo anataka kugombea tena.

Hatua ya Boris Johnson kugombea uongozi wa chama na kuwa waziri mkuu umekigawanya chama cha Conservative, ambacho kimewafukuza mawaziri wakuu 4 katika muda wa miaka sita.

Baadhi ya wanachama wa Conservative wanasema kwamba Boris anastahili kupewa nafasi nyingine, kutokana na ushawishi wake kote nchini.

Boris alijiuzulu kutokana na kile kilichothibitishwa 'kusema uongo', na maafisa wake katika serikali walikumbwa na sakata mbalimbali zikiwemo ulevi.

XS
SM
MD
LG