Gabon inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka huu.
Maandamano mabaya yalitokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 baada ya Bongo kutangazwa mshindi. Waandamanaji walidai kwamba Bongo alikuwa amefanya udanganyifu na ushindi wake haukuwa halali.
Pendekezo la kupunguza muda wa mhula wa rais linahitaji kufanyiwa mabadiliko ya kikatiba na kupigiwa kura katika bunge.
Bongo, mwenye umri wa miaka 64, amekuwa rais wa Gabon, ambayo inaalisha mafuta tangu mwaka 2009, alipofariki babake, rais Omar Bongo.
Hajasema iwapo atagombea mhula wa tatu madarakani mwaka huu 2023.
Tarehe ya uchaguzi mkuu haijatangazwa.
Hakuna kikomo cha mhula kwa wagombea wa urais nchini Gabon.
Facebook Forum