Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:28

Bondia Mayweather akabiliwa na mashitaka


Bondia Mmarekani Floyd Mayweather Jr. akabiliwa na mashitaka yanayoweza kumpeleka gerezani miaka 30.

Bondia Floyd Mayweather Jr. wa Marekani ambaye hajawahi kupoteza hata pambano moja anakabiliwa na mashitaka maneno ya jinai, ikiwa ni pamoja utumiaji nguvu nyumbani na wizi, mashitaka yanayoweza kumpeleka gerezani kwa miaka 30.

Maafisa katika mji wa Las Vegas, Nevada, wiki hii wamemfungulia Mayweather mashitaka manne ya jinai na mengine manne madogo. Mashitaka hayo yanatokana na ugomvi uliotokea karibu mara mbili usiku wa manane katika nyumba ya rafiki wake wa kike wa zamani, Josie Harris, ambaye ni mama wa watoto watatu kati ya watoto wanne wa bondia huyo mwenye umri wa miaka 33. Mayweather ndiye anayemiliki nyumba hiyo.

Mashitaka yote yatategemea na tathmini ya waendesha mashitaka. Si Mayweather wala wakili wake ambao wamepatikana kusema lolote kuhusu madai hayo. Bondia huyo yuko huru kwa dhamana tangu kukamatwa kwake Ijumaa ya Septemba 10, 2010 mpaka atakapofikishwa mahakamani Novemba 9, 2010.

XS
SM
MD
LG