Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 17:26

Bomu lalipuka kwenye basi Pakistan


Picha ya baadhi ya watu wakiwa kwenye basi

Uchunguzi wa awali wa polisi ulieleza kwamba vifaa vilivyosababisha mlipuko vilifichwa chini ya kiti na kifaa cha kutegua bomu kwa muda maalum kilitumika.

Bomu moja limelipuka ndani ya basi lililojaa abiria huko kaskazini-magharibi mwa Pakistan leo Jumatano na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 15 na kuwajeruhi watu wasiopungua 30 wengine.

Waathirika wengi ni wafanyakazi wa serikali, kwa mujibu wa maafisa wa jimbo katika mji wa Peshawar, eneo lililotokea mlipuko huo.

Uchunguzi wa awali wa polisi ulieleza kwamba vifaa vilivyosababisha mlipuko vilifichwa chini ya kiti na kifaa cha kutegua bomu kwa muda maalum kilitumika. Picha za televisheni zilionesha mlipuko huo ulokua mbukwa uliharibu kabisa basi la abiria.

XS
SM
MD
LG