Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:57

Wanajeshi 6 wauwawa kwa bomu mpakani mwa Jordan na Syria


Afisa wa jeshi la Jordan anasema bomu lililotegwa kwenye gari limelipuka katika mpaka wa Jordan na Syria na kuwaua wanajeshi sita na kujeruhu wengine 14.

Taarifa ya jeshi la Jordan imeeleza kwamba mlipuko umetokea katika eneo la Rukban, mita mia kadhaa kutoka kwenye kambi ambapo mamia elfu ya watu waliokimbia ghasia nchini Syria wanaitumia kuombea ukimbizi wakati wakijaribu kuingia nchini Jordan.

Hakuna kundi lolote ambalo limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Jeshi la Jordan linasema bomu hilo limeharibu magari kadhaa ambayo yalihusika lakini likashindwa kutoa taarifa zaidi.

XS
SM
MD
LG