Shirika la habari la ufaransa 'AFP' linaripoti kwamba watu 6 waliuwawa mapema leo baada ya bomu la kujitoa muhanga kulipuka katika msikiti wa Damboa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, kanali Sani Usman, amesema shambulizi hilo lilitokea asubuhi katika mji uliopo kilometa 90 kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri.
Msemaji huyo amesema shambulizi hilo limefanywa na wanamgambo wa Boko Haram.
Shambulizi la kwanza lilikuwa limepangwa kufanyika katika msikiti wa katikati ya mji wa Damboa, lakini kutokana na ulinzi mkali, mjilipuaji alijiua na bomu na kuuwa waumini wengine 6 na kumjeruhi mtu mmoja.