Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 19, 2025 Local time: 01:49

Bomu laua watu wawili Somalia


Mlipuko wa bomu Somalia.
Mlipuko wa bomu Somalia.

Raia wawili akiwemo mtoto wa kike wa miaka saba wameuawa na mlipuko wa bomu katika mji wa Kismayo upande wa bandari ya kusini jioni Ijumaa, maafisa wa serikali ya Somalia wameiambia VOA.

Mripuko huo umetokea wakati mtu aliyekuwa amevaa mkanda wenye mabomu kujilipua wakati vikosi vya ulinzi vilipokuwa vikimzuia kuingia katika kambi ya kijeshi.

Mtu aliyeshuhudia tukio hilo amesema mtu huyo alijaribu kuingia ndani ya gari lililokuwa limebeba wanajeshi na gari likachomoka haraka.

Mtu huyo baadae aligeuka na kulipua mabomu na kujiua yeye mwenyewe na raia wawili.

Wakati huo huo mmoja wa kiongozi wa kijadi jijini Mogadishu aliyeshiriki katika mchakato wa uchaguzi wa Somalia alipigwa risasi na kuuawa na anayeshukiwa kuwa mpiganaji. Kiongozi huyo ametambuliwa kwa jina la Abdi Dhore na ni mzee wa tatu kuuwawa Mogadishu katika siku tatu.

Hata hivyo kumekuwa hakuna tamko lolote kutoka kwa Al-Shabab kuhusu mauaji ya leo lakini kikundi hicho cha wapiganaji kinalaumiwa kwa kulenga kuwaua wabunge, wawakilishi, viongozi wa jadi, wafanyakazi wa serikali, polisi wa barabarani, wakusanyaji kodi, wapelelezi, wafanyabiashara, wanaharakati wa asasi za kijamii, na waandishi.

XS
SM
MD
LG