Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:28

Shambulizi la bomu laua watu 8 Burundi


Ramani ya Burundi
Ramani ya Burundi

Afisa wa Serikali ya Burundi amesema watu wanane wameuawa katika shambulizi la bomu la mkono lililotupwa ndani ya baa katika eneo la kijijini la nchi hiyo upande wa kaskazini.

Devote Ndayizeye ambaye ni Kiongozi wa Gatara commune katika jimbo la Kayanza ambapo shambulizi hili lilitokea Jumapili usiku, amesema watu wawili walipoteza maisha kutokana na majiraha baada ya kulazwa hospitali, limeripoti shirika la habari la AP

Ndayizeye amesema washambuliaji hao walikimbia kutoka sehemu hiyo ya tukio na sababu za uhalifu huo hazijaweza kujulikana.

Burundi imeingia katika balaa la uvunjifu wa amani wa hapa na pale tangu April 2015 wakati Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kuendelea na awamu ya tatu katika uongozi, jambo lililopelekea maandamano makubwa nchini humo.

Nkurunziza alishinda awamu nyingine ya uongozi katika uchaguzi uliokuwa na utata Julai 2015 na ameendelea kuwa madarakani na Burundi imekuwa katika hali isiyo ya utulivu.

Angalau kundi moja la wapiganaji limetangaza uasi na kuendeleza mashambulizi jambo linalotishia kurejea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

XS
SM
MD
LG