Mtu mmoja alijeruhiwa mkononi na bomu hilo ambalo polisi wamesema lilitengenezwa kwa kutumia fataki.
Mlipuko huo ulitokea karibu na eneo ambapo watu wanao omba visa wanajipanga kuingia ubalozini kwa ajili ya usaili.
Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii baada ya mlipuko huo zilionyesha wingu kubwa la moshi lilofunika eneo la ubalozi katika mji mkuu wa China.
Ubalozi uko katika eneo la Beijing ambalo kuna ofisi za ubalozi kadhaa, ikiwepo ya India na Israel.
Gazeti la Global Times linalo endeshwa na serikali mapema Alhamisi limesema polisi walikuwa wamemkamata mwanamke karibu na ubalozi wa Marekani ambaye alikuwa amejilowesha kwa petroli ikiwa inashukiwa kuwa alikuwa anajaribu kujitoa muhanga.